Cristiano Ronaldo amesimulia kisa cha kwenda kumtoa jukwaani na kumkumbatia shabiki ambaye wengi walijiuliza ana uhusiano naye gani baada ya ushindi wa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Ronaldo alisema “Ni lazima nimshukuru rafiki yangu Albert Fantrau kwa mafanikio ninayoyapata. Tulicheza pamoja katika klabu ya vijana. Walipokuja watu kutoka Sporting Lisbon, walisema yeyote atakayefunga magoli mengi atachukuliwa na Academy.”
“Tulishinda mechi hiyo 3 – 0, nilifunga goli la kwanza, kisha Albert akafunga goli la pili kwa kichwa, na la tatu ndilo lililomvutia kila mmoja. Albert alikwenda kukutana uso kwa uso na kipa. Nilikuwa nakimbia pembeni yake, akampiga chenga kipa, alichohitaji ni kutumbukiza tu mpira wavuni kwani lango lilikuwa tupu. Lakini, akanipasia mimi nikafunga. Nikachukuliwa kwenda kwenye Academy.”
“Baada ya mechi nilimfuata na kumuuliza “Kwanini ulifanya vile Albert?” akanijibu kuwa “Ronaldo, wewe ni bora zaidi yangu”. Ni kauli iliyonitoa machozi na ninaishi nayo hadi leo.
Albert Fantrau alipoulizwa kuhusu habari hii ya Ronaldo alisema “ni kweli ndicho kilichotokea”. Aidha, alipoulizwa kuhusu utajiri alionao, ikiwa ni pamoja na nyumba yake ya kifahari na uwezo wa kuilea familia yake ilhali hana kazi ya maana Albert alisema
“Ni kutoka kwa Cristiano.”

Post a Comment