Mgomo wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia umesababisha hasara ya Sh bilioni 2.65 ambazo sasa Serikali imesema wafanyakazi watakatwa kwenye mishahara yao kufidia.
Wafanyakazi hao ambao jana wametangaza kusitisha mgomo huo baada ya Mahakama kuubatilisha juzi, imeelezwa kwamba mishahara yao itakatwa kwa utaratibu utakaowekwa na Menejimenti.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alisema mgomo huo ulioanza Mei 12 mwaka huu, umesababisha hasara ya dola za kimarekani milioni 1.6 sawa na Sh bilioni 2.65.
Awali, Dk Mwakyembe alitaka wafanyakazi hao kutii amri ya Mahakama kwa kurejea kazini na kusema atakayekaidi atakuwa amejifukuzisha.

Post a Comment