Polisi imesema imekamata watu 17, wanaotuhumiwa kuhusika na ulipuaji wa mabomu jijini Arusha na usajili wa vijana kwa lengo la kuwasafirisha kwenda nje ya nchi, kujiunga na vikundi vya kigaidi ikiwemo Al shabab.
Pia, watu hao wanatuhumiwa kutaka kulipua maeneo mengine, hasa taasisi za Serikali na maeneo ya mikusanyiko ya watu.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI), Isaya Mungula alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari jijini Arusha, muda mfupi kabla ya watuhumiwa kufikishwa na kusomewa mashitaka hayo mahakamani.Mungula alisema kukamatwa kwa watu hao, kunatokana na tukio la Aprili 13 mwaka huu saa 1.30 usiku katika baa ya Arusha Night Park .

Post a Comment