Mshambuliaji
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anachechezea
klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yuko katika
mipango ya kuhamia Ulaya. Taarifa za uhakika zinasema Samatta tayari
ameshamtaarifu uamuzi wake huo tajiri wa timu hiyo, Moisse Katumbi
Chapwe, ambaye amekubaliana naye.
Aidha, pamoja na kutokutaka
kkuelezea klabu za Ulaya zinazomuwania Samatta amedokeza kuwa anatarajia
kucheza Ufaransa, Ureno au Ubelgiji kulingana na makubaliano
yatakavyofikiwa.
Post a Comment