0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Michezo ya nane ya Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itafanyika Zanzibar kuanzia Agosti 18, mwaka huu. 
Akitoa Taarifa ya Mkuu wa Majeshi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  Makao Mkuu ya Brigedi Migombani kwa waandishi wa Habari, Mkuu wa Brigedi hiyo Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman amesema lengo la michezo hiyo  ni kujenga  mashirikiano kati ya Majeshi na Jumuiya ya Afrika Mashariki
Amesema katika Michezo hiyo kutakuwa hakuna mshindi wala aliyeshindwa na wote watakuwa washindi, lengo ni kujenga uweledi na nidhamu ndani ya majeshi yetu.

Mkuu wa Bregedi ya Nyuki ambae ni Makamo Mwenyekiti wa michezo ya Majeshi Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman akizungumza na waandishi wa habari kuhusu michezo ya nane ya Majeshi ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Mkuta huo umefanyika huko Bregedi ya Nyuki Migombani Zanzibar.

“Hii ni fursa ya wanajeshi wetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana pamoja kama tunavyofanya katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi”, alisema Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman.
Amezitaja Nchi za Jumuiya hiyo zitakazoshiriki  Michezo hiyo kuwa ni wenyeji Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya  na Uganda.
Amesema Michezo itakayochezwa na wanajeshi hao ni  Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Mikono, Mpira wa Kikapu  na Mbio za nyika  na ameelezea viwanja vitakavyofanyika kwa ajili ya michezo hiyo  Polisi ziwani ,Vyuo vya Mfunzo Kilimani, JKU Saateni, Pamoja na Viwanja vya Zimamoto na Uokozi.
Brigedia Jenerali Sharif Sheikh ambaye pia ni Makamo  Mwenyekiti wa Michezo hiyo, amewataka  Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuona vipaji vitakavyoonyeshwa na wanajeshi kutoka Nchi hizo .
Akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo Leftinenti Kanali Joseph Bakari amesema pamoja na micheo hiyo kutakuwa na Burudani ya Ngoma za Utamaduni kutoka Vikosi vya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema jumla ya wanamichezo 505 wakiwemo Viongozi kutoka Nchi hizo watashiriki michezo hiyo itakayodumu kwa muda y

Post a Comment

 
Top