Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi
wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe
la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa
timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya
mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha
kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao
kuiwasilisha kwa CECAFA.
“Baada ya kuthibitisha kushiriki
michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na
viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo
ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho
tulitimiza” alisema Beno.
“Lakini katika hali ya kushangaza jana
tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano
hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua
nafasi yetu ati kwa vile katika timu yetu tumepeleka wachezaji wa timu
B,” aliongeza Beno.”
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji
wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za kucheza
mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo orodha
tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda
kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014
kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi
ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua
na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na
wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado
Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi
timu nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na
hata kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka
majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa
maelekezo ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga
na klabu ya Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka
katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10
wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa
Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa
Agosti, takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa
kupumzika.
c) Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha
mkuu Maximo na wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda
na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji
waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha kwenye kikosi
cha kwenda Kigali Rwanda.
d) Baadhi ya wachezaji wanahitaji
Vibali vya kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza
kushiriki michuano ya Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA mchezaji
anayeshiriki mashindano hayo ni lazima awe na leseni ya kucheza mpira
kwa ligi ya ndani.
e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa
kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika
kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20
kuwa watano tu.
f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa
takribani miezi mitatu bila ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate
japo siku kumi na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa na
kuanza upya tena maandalizi ya msimu mpya.
g) Yangga tunaamini
hakuna mtu yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha
kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora
wa wachezaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment