0
Yanga SC itashuka tena dimbani Jumapili kumenyana na Bata Bullets ya Malawi katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Huo utakuwa mchezo wa tano chini ya kocha mpya, Mbrazil Marcio Maximo baada ya awali kushinda mechi zote nne, 1-0 mara mbili dhidi ya Thika United ya Kenya na Chipukizi ya Pemba na 2-0 mara mbili dhidi ya Shangani na KMKM zote za Zanzibar. Yanga SC imetoa wito kwa mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo Jumapili kuipa sapoti timu yao. 

Post a Comment

 
Top