0
Kipimo Abdallah
WANACHAMA 75 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Msasani Jimbo la Kawe akiwemo Katibu Mwenezi wa Baraza  la Wanawake Chadema Kawe  (BAWACHA) wamejiunga na chama cha Alliance for Change and Transparent (ATC-Tanzania).
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa ACT-Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam Khamis Chambuso wakati akiwakabidhi kadi za chama hicho leo jijini Dar es Salaam.Chambuso alisema wanachama hao pamoja na wanachama wengine kutoKA Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CHAUMA wamejiunga na ACT- Tanzania kwa mapenzi yao bila kushawishi na kitu chochote.
Alisema kwa siku jana wamepokea wanachama 78 ambapo mmoja anatokea mkoa wa Kigoma na wengine wanatokea mkoa wa Dar es Salaam wengi wao wakiwa ni kutoka CHADEMA.

Post a Comment

 
Top