Katika ratiba ya michuano hiyo iliyopangwa leo mjini Kigali, KMKM ya Zanzibar ambayo ipo kundi moja A na Yanga, itafungua pazia la michuano hiyo mchana wa siku hiyo kwa kumenyana na Atlabara ya Sudan Kusini.

Yanga itaanza na Rayon Kombe la Kagame |
Yanga SC itarudi tena dimbani, Agosti 10 kumenyana na jirani zao KMKM, kabla ya kucheza na Atlabara Agosti 12 na kukamilisha mechi za kundi lake, kwa kumenyana na Coffee ya Ethiopia Agosti 16.
Wawakilishi
wa Tanzania, Yangs SC wanatarajiwa kuingia kambini Agosti 1, mwaka huu
kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya 40.
Yanga SC inayofundishwa Marcio Maximo anayesaidiwa Leonardo Neiva, wote Wabrazil na mzalendo Salvatoty Edward, imetwaa mara tano taji la michuano hiyo, 1975 visiwani Zanzibar, 1993 na 1999 mjini Kampala, Uganda na mara mbili mfululizo pia 2011 na 2012 mjini Dar es Salaam.
Maana yake watakwenda Kigali mwezi ujao kujaribu kusawazisha rekodi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliotwaa mara sita, 1974, 1991 mjini Dar es Salaam, 1992 visiwani Zanzibar, 1995, 1996 mjiji Dar es Salaam na 2002 Zanzibar tena.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano haya ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawadi.
Wizara ya Michezo ya Rwanda na mashirika mengine yatadhamini michuano hiyo, itakayokwenda sambamba na maazimisho ya miaka 20 ya mauwaji ya kimbau.
Televisheni ya kulipia ya Supersport ya Afrika Kusini ambao ni maswahiba wa muda mrefu wa CECAFA, ni miongoni mwa wadhamini pia na wataonyesha mechi zote za michuano hiyo moja kwa moja.

Post a Comment