0
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imelazimishwa sare ya bila kufungana na Afrika Kusini, Amajimbos katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanamaanisha, Serengeti Boys itahitaji sare ya mabao katika mchezo wa ugenini, au kushinda kabisa ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo katika kuwania tiketi ya Fainali zitakazopigwa Niger mwakani.
Amajimbos waliuanza mchezo vizuri wakilitia kwenye misukosuko lango la Serengeti kwa dakika takriban 20 za mwanzo, lakini taratibu mchezo ulianza kubadilika na wenyeji wakageuza kibao

Post a Comment

 
Top