0
CAIRO, Misri
MOROCCO itakosa Fainali mbili zijazo za Mataifa ya Afrika (Afcon) kama adhabu ya kukataa ghafla kuandaa michuano hiyo mwakani, imefahamika.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou alikaririwa jana na gazeti la michezo la kila siku nchini Ufaransa, ‘France’s L’Equipe sports daily’ akisema: “Tutabaki katika misingi ya sheria, ambayo inamaanisha kuondolewa katika michuano miwili ya Mataifa ya Afrika,” alisema Hayatou na kuongeza;
“Na juu ya hilo watapigwa faini ya fedha.”
moro
Morocco wanakabikiwa na faini ya dola za Kimarekani milioni 20 kwa kukataa ghafla kuwa wenyeji wa Afcon 2015 inayotarajiwa kuanza Januari 17 hadi Februari 8, baada ya kukataa uenyeji kwa kuhofia kuenea kwa Ebola.
Matajiri wa mafuta, Equatorial Guinea, ambao waliandaa kwa pamoja na Gabon Afcon 2012 walitajwa kuchukua nafasi ya Morocco ya uenyeji wa michuano hiyo

Post a Comment

 
Top